Posts

Showing posts from December, 2018

Mwanamke na Uongozi

Image
Na: RIDHAA KORONGO Miaka ya nyuma nchini Tanzania, wanawake hawakuwa wakipewa kipaumbele katika uongozi. Hata hivyo, hivi karibuni serikali na jamii zimetambua mchango wa wanawake, na hivyo kuanza kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi, si tu serikalini bali pia katika taasisi zisizo za kiserikali. Hata hivyo, bado wapo baadhi ya watu wanaoamini kuwa wanawake hawawezi kushika nyadhifa za uongozi kutokana na changamoto wanazokumbana nazo. Wengi wa watu hawa hawajui kuhusu Mtawala wa kike aliyerithi uchifu baada ya baba yake kufariki dunia. Leo, kalamu yangu inawaandikia juu ya Mwami Theresa Ntare VI, aliyezaliwa mwaka 1926 na kufariki mnamo tarehe 23 Mei 1993 akiwa na umri wa miaka 67. Theresa alikuwa mtawala wa kike aliyerithi uchifu baada ya baba yake, Mwami Gwasa, kufariki dunia. Alikabidhiwa uchifu kwa sababu hakuwa na kaka wa kurithi nafasi hiyo katika familia yao. Kinyume na mila zilizotaka kutafutwa mtoto wa kiume kutoka kwa ndugu wengine, Bi. Theresa alipewa nafasi hiyo, na hi...