Posts

Unyanyasaji wa Kijinsia

Nimekuandalia makala fupi kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa wasichana. Mara nyingi tumekuwa tukisikia kesi mbalimbali za wanawake kunyanyaswa na waume zao, lakini je, wasichana hawakumbwi na unyanyasaji kutoka kwa wapenzi wao wakiwa kwenye mahusiano kabla ya ndoa? Karibu usikilize makala haya yaliyoandaliwa na kusimuliwa na RIDHAA KORONGO.

Mwanamke na Uongozi

Image
Na: RIDHAA KORONGO Miaka ya nyuma nchini Tanzania, wanawake hawakuwa wakipewa kipaumbele katika uongozi. Hata hivyo, hivi karibuni serikali na jamii zimetambua mchango wa wanawake, na hivyo kuanza kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi, si tu serikalini bali pia katika taasisi zisizo za kiserikali. Hata hivyo, bado wapo baadhi ya watu wanaoamini kuwa wanawake hawawezi kushika nyadhifa za uongozi kutokana na changamoto wanazokumbana nazo. Wengi wa watu hawa hawajui kuhusu Mtawala wa kike aliyerithi uchifu baada ya baba yake kufariki dunia. Leo, kalamu yangu inawaandikia juu ya Mwami Theresa Ntare VI, aliyezaliwa mwaka 1926 na kufariki mnamo tarehe 23 Mei 1993 akiwa na umri wa miaka 67. Theresa alikuwa mtawala wa kike aliyerithi uchifu baada ya baba yake, Mwami Gwasa, kufariki dunia. Alikabidhiwa uchifu kwa sababu hakuwa na kaka wa kurithi nafasi hiyo katika familia yao. Kinyume na mila zilizotaka kutafutwa mtoto wa kiume kutoka kwa ndugu wengine, Bi. Theresa alipewa nafasi hiyo, na hi...

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Image
Na: Ridhaa Korongo Pampasi ya kwanza ilianza kutumika mnamo mwaka 1961 nchini Marekani, baada ya wazo la kutengeneza pampasi kutolewa na Mmarekani Victor Mills mwaka 1956. Hii ilitokana na kuchoshwa kwake na kazi ya kubadili nepi za mjukuu wake. Tangu wakati huo, pampasi zimeenea duniani kote, zikiwapa wazazi njia rahisi zaidi ya kudhibiti haja za watoto. Hapa Tanzania, pampasi zilianza kutumika mapema miaka ya 2000 na zimeendelea kushamiri, hasa katika maeneo ya mijini. Kwa sasa, pampasi zimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya wazazi, zikichukua nafasi ya mipira, nepi, na matambara yaliyokuwa yakitumiwa zamani. Wakati huo, kila mzazi alihitaji kuchana vipande vya kanga au kununua nepi kwa ajili ya watoto wao. Lakini siku hizi, imekuwa kawaida kwa kila familia yenye mtoto kuwa na pampasi, ambayo sasa hutumika kama “nguo ya ndani” kwa watoto, ikisaidia kuzuia kinyesi na mkojo kutapakaa. Ingawa pampasi zimewasaidia wazazi kwa kuwaondolea kazi kubwa ya kufua nepi na matambara ma...

Magazeti ya leo, Jumapili Julai 24

Image

Haya Hapa magazeti ya leo Julai 2 2016

Image

KLOPP AMNASA MANE

Image
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Southampton Sadio Mane hatimaye baada ya tetesi za muda mrefu amesaini kandarasi ya miaka 5 na majogoo wa Anfield Liverpool kwa ada ya paundi ml 34. Mane anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Liverpool msimu huu, Klopp ameshafanya usajili wa Joel Matip na kipa Loris Karius. Klopp ameonyesha nia ya dhati ya kuwa na safu ya ushambuliaji iliyoshiba tayari yenye majina kama Benteke, Sturridge na Origi. Kwa usajili huu mashabiki wa Liverpool wanazidi kuwa na imani ya klabu yao kufanya vizuri msimu ujao ikikumbukwa Klopp aliifikisha fainali za Europa na Capital one cup bila usajili wowote.

UINGEREZA AIBU, HODGSON ATIMUA

Image
Timu ya taifa ya Uingereza ' The three Lions' imeaga fainali za EURO zinazoendelea Ufaransa baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Iceland. Uingereza ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa mshambuliaji wa Mashetani wekundu Wayne Rooney 'Wazza' dakika ya 4 kwa njia ya mkwaju wa penalti, lakini Iceland wakarudi mchezoni na kusawazisha dakika ya 6 kupitia kwa Sigurdsson na kumalizia la pili dakika ya 16 kupitia kwake Sigthorsson. Matokeo haya ya kushangaza yanamaanisha Iceland watakipiga na  Ujerumani hatua ya robo fainali baada ya kuwatoa Slovakia. Ikumbukwe mapema mwa mashindano haya Chief wa shirikisho la mpira nchini Uingereza FA bwana Greg Dyke alisema kwamba kocha mkuu Roy Hodgson atatimuliwa endapo atashindwa kuifikisha Uingereza nusu fainali. Basi kufuatia kutolewa kwa Uingereza Hodgson bila ya kutimuliwa ameamua kujivua kama kocha mkuu wa Uingereza.