UINGEREZA AIBU, HODGSON ATIMUA
Timu ya taifa ya Uingereza ' The three Lions' imeaga fainali za EURO zinazoendelea Ufaransa baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Iceland.
Uingereza ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa mshambuliaji wa Mashetani wekundu Wayne Rooney 'Wazza' dakika ya 4 kwa njia ya mkwaju wa penalti, lakini Iceland wakarudi mchezoni na kusawazisha dakika ya 6 kupitia kwa Sigurdsson na kumalizia la pili dakika ya 16 kupitia kwake Sigthorsson.
Matokeo haya ya kushangaza yanamaanisha Iceland watakipiga na Ujerumani hatua ya robo fainali baada ya kuwatoa Slovakia.
Ikumbukwe mapema mwa mashindano haya Chief wa shirikisho la mpira nchini Uingereza FA bwana Greg Dyke alisema kwamba kocha mkuu Roy Hodgson atatimuliwa endapo atashindwa kuifikisha Uingereza nusu fainali.
Basi kufuatia kutolewa kwa Uingereza Hodgson bila ya kutimuliwa ameamua kujivua kama kocha mkuu wa Uingereza.

Comments
Post a Comment