MZEE WENGER AHAHA

Baada ya kumkosa Jamie Vardy aliyeongeza mkataba na Leicester City sasa kocha mkuu wa Arsenal the gunners washika bunduki Aresene Wenger, anahamishia nguvu kwa kiungo wa Leicester N'golo Kante.




Vardy alikataa kutua Emirates waliokuwa wakitaka kumnunua kwa kitita cha paundi millioni ishirini na kubaki King power stadium baada ya kuongezewa mshahara kufikia paundi laki moja kwa wiki.

Kwa miaka ya karibuni, Wenger amekuwa na historia ya kupokonywa tonge mdomoni kwa upande wa washambuliaji akikosa washambuliaji hatari kama Luis Suarez, Gonzalo Higuain, Wayne Rooney, Karim Benzema na sasa Jamie Vardy.



Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia