SERIKALI YASITISHA HUDUMA ZA VYAKULA MUHIMBILI
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesitisha zoezi la utoaji chakula kwa wagonjwa hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka hapo serikali itakapojiridhisha faida na hasara ya zoezi hilo.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa amefikia maamuzi hayo baada ya kupokea maoni kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Muhimbili imeanzisha utaratibu utakaowezesha wagonjwa kuchangia gharama ya chakula ili chakula kiweze kuandaliwa na hospitali badala ya utaratibu wa sasa.
Waziri huyo ameagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpaka hapo zitakapopatikana taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu huo mpya uliopendekezwa.
Waziri huyo ameagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpaka hapo zitakapopatikana taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu huo mpya uliopendekezwa.
Comments
Post a Comment