CR7 KWA MBINDE ROBO FAINALI EURO

Imechukua dakika 30 za nyongeza ndipo Portugal walipoweza kuchomoza na ushindi finyu wa bao moja, bao lililofungwa na Ricardo Quaresma mnamo dakika ya 117 ya mchezo.


Matokeo hayo yanaipeleka Ureno robo fainali wakikutana na Poland walioitoa Switzerland kwenye mechi nyingine iliyopigwa mapema usiku wa leo.

Ni robo fainali inayosubiriwa kwa hamu ikikutanisha washambuliaji wawili wenye majina na mafanikio katika klabu zao, Cristiano ronaldo 'CR7' anyekipiga Real Madrid kwa Ureno na Robert Lewandowski anayekipiga kunako Bayern Munchen 'The Bavarians'.

Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia