KADI ZA USAFIRI WA MABASI YA MWENDO KASI ZATOLEWA RASMI

Kadi za elektroniki kwa usafiri wa mabasi ya mwendo kasi zimezinduliwa jijini Dar es salaam. 

Awali baadhi ya watu wali was il is ha malalamiko kadha wa kadha kwa Mkuu wa Mkoa juu ya msongamano wa watu na usumbufu unaotokea wakati wa kukata tiketi za mabasi hayo.

Wauzaji wa tiketi hizo Max malipo na Shirika la Usafiri la Dar es saalam UDA wamesema tiketi hizo za kieletroniki zitauzwa katika vituo vikubwa kwa shilingi elfu tano. Mnunuzi atahitajika kujisajili na kuweka fedha ndani ya kadi yake. Tamko lilitolewa kuwa kwa usajili huo, endapo kadi itapotea, akiba ya fedha iliikuwa imebaki itaingizwa kwenye kadi mpya atakayopewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa UDART Bw.David Mgwassa, amesema kadi hizo zitaanza kuuzwa leo katika vituo vikuu vya mabasi vya kimara, Ubungo, Morocco , Gerezani na Kivukoni.

Kwa upande wake Kampuni ya Max Malipo ilitoa tamko kuwa kadi zitauzwa kwa bei ya shilingi 5000, na itakuwa na 4500 ndani take ambazo zitamwezesha abiria kutumia kama nauli kwa safari nane. Waliendelea kusema Kadi hizo hazitakuwa na namba ya siri na kiwango cha juu kitakachoweza kuwekwa ndani ya kadi hio ni tshs 30,000.

Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia