SPAIN HOI NORTHERN IRELAND YAPENYA

Katika mwendelezo wa mashindano ya EURO, mechi za kundi D zimepigwa na Spain wamefungwa goli 2-1 na Croatia, huku Alvaro Morata ambaye anarudi Real Madrid msimu ujao kutoka Juventus akifungua kitabu cha magoli mnamo dakika ya 7.



Nahodha na beki wa Real Madrid Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penalti mnamo dakika ya 72 ya mchezo baada ya David Silva kufanyiwa madhambi na Sime Vrsaljko.

Croatia walirudi mchezoni kupitia kwake Nikola Kalinic dakika ya 45 huku Ivan Perisic akiwakata maini Spain kwa kufunga goli la lalasalama na la ushindi dakika ya  87 ya mchezo.





Matokeo haya yameifanya Croatia kuwa vinara wa kundi D wakiwa na pointi 7 huku Spain wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 6 nao Uturuki wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 3 baada ya kupata ushindi wa kwanza baada ya kupoteza michezo yao miwili ya awali.


Uturuki watakipiga jumamosi hii na moja ya timu zilizoshika nafasi ya tatu kutoka kundi B, E au F huku spain wao wakikutana na timu ya taifa ya taifa ya Italy 'Azzuri' ikiwa ni ukumbusho wa fainali hizi za Euro mwaka 2012 ambapo Spain walipata ushindi wa goli 4-0.




Uturuki ikiongozwa na Arda Turan imepata ushindi wa 2-0 dhidi ya Czech Republic, magoli yakifungwa na Burak Yilmaz dakika ya 10 na Ozan Tufan kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 65.

Ushindi huu umeiweka Uturuki kwenye nafasi ya tatu kundi D huku wakiwa na matumaini ya kupata nafasi ya 'best loser', Northern Ireland waliofungwa kwenye mechi iliyopigwa awali na kufungwa na Ujerumani wamepita hatua ya 16 bora kwa nafasi ya 'best loser' wakiwapiku Uturuki kwa tofauti ya magoli wote wakiwa na pointi 3.



Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia