GOMEZ AIBEBA UJERUMANI 16 BORA

Ujerumani yapenya hatua ya 16 bora baada ya ushindi mwembamba wa goli moja bila majibu dhidi ya Northern Ireland, goli lililofungwa na mshambuliaji Mario Gomez dakika 30 ya mchezo.



Kwa matokeo hayo Ujerumani inatinga hatua ya 16 bora ikiwa kama kinara wa kundi C ikiwa na pointi 7 ikifuatiwa na Poland nayo yenye pointi 7, ikishika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya magoli.

Northern Ireland inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 3 ikisubiria nafasi za washindi wa tatu bora kwenye makundi yote ama maarufu kama 'best loser', ambayo kwa sasa wako nafasi ya pili nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Slovakia wanaoshika nafasi ya tatu kwenye kundi B wakiwa na pointi 4, nafasi hizo zipo nne tu.





Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia