Mtoto wa Afrika
Leo Tarehe 16 Juni ni siku ya mtoto wa Afrika ambayo hua inaadhimishwa kila mwaka ikiwa kama ni kumbukumbu ya wote walopoteza maisha na waliomia mwaka 1976 Soweto.
Siku hii imekua ikiadhimishwa kila mwaka tangu Umoja wa Afrika (AU) ulipoianzisha rasmi mwaka 1991.
Historia fupi ya siki hii
Tarehe 16 juni 1976 kwenye mji wa Soweto nchini Afrika ya kusini maelfu ya wanafunzi wa kiafrika waliandamana kwenye mistari wenye urefu ambao vitabu vimeandika kua ulifikia mita mia tano au zaidi wakipinga elimu duni wanayoipata kutoka kwa serikali ya Makaburu na pia walikua wakidai haki ya kufundishwa kwa lugha zao za asili na sio kikaburu.
Wanafunzi wengi walipigwa risasi, mmoja wapo akiwa ni Hector Pieterson. Baada ya wiki mbili yalifanyika maandamano mengine ambapo zaidi ya watu mia moja waliuawa kwenye maandamano hayo na maelfu walijeruhiwa.
PICHA: Hii picha ilipigwa na mpiga picha SAM NZIMA ikimuonesha MBUYISA akiwa HECTOR PIETERSON (akiwa amepoteza maisha) na pembeni ni dada yake ANTOINETTE SITHOLE.
Tarehe 16 juni kila mwaka, Serikali, mashirika ya uma, asasi zisizo za kiserikali, makampuni na wadau wengine wanakutana pamoja kujadili changamoto zinazoakumba watoto wa Afrika.
Kwa Dar es Salaam maadhimisho hayo yanayanyika leo katika viwanja vya Mwembe yanga mgeni rasmi akiwa ni Mheshimiwa Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na kauli mbiu ikiwa ni "TOKOMETA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI PAMOJA TUNAWEZA.
Comments
Post a Comment