UBELGIJI YAPETA URENO YABANWA

Timu ya taifa ya Ubelgiji imeonyesha makali yake baada ya kuwachapa jamhuri ya Ireland kwa jumla ya magoli 3-0 huku mshambuliaji kutoka klabu ya Uingereza ya Everton the toffees akiwa mwiba mkali baada ya kufunga mabao mawili akifungua kitabu cha magoli mnamo dakika ya 48 ya mchezo huku Witsel akifunga la pili dakika ya 61 na Lukaku tena kwa mara nyingine kufunga goli lake la pili na la tatu kwa Ubelgiji na kupunguza uwezekano wa Ireland kuvuka hatua ya makundi.

                                                     Lukaku akishangilia moja ya goli lake

Nao Ureno Ikiwa ni mechi yao ya pili kwenye mashindano ya UERO mwaka huu na mechi ya 128 kwa captain wao Cristiano Ronaldo CR7 Ureno yabanwa mbavu na Austria kwenye mchuano mwingine.

Cristiano ronaldo alikosa penalti kwenye mechi hii akiwa mchezaji wa kwanza wa Ureno kukosa penalti ndani ya dakika za kawaida.

Matokeo haya yanaiweka Ureno nafasi ya tatu ikiwa na pointi 2 ikitanguliwa na Iceland yenye pointi 2 na kiongozi wa kundi hilo F wakiwa na pointi 4.



Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia