ARGENTINA FAINALI COPA AMERICA
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona Lionel Messi ameiongoza Argentina kupata ushindi wa goli 4-0 dhidi ya wenyeji Marekani baada ya kutoa pasi ya mwisho ya goli la la Ezequiel Lavezzi dakika ya 3 na kufunga freekick maridadi iliyomshinda kipa wa Aston Villa Brad Guzan.
. Magoli mengine mawili yalifungwa na straika wa SSC NAPOLI, Gonzalo Higuain mnamo dakika ya 50 na ya 86 ya mchezo na kuiwezesha Argentina kutinga hatua ya fainali ya kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.
Argentina walitinga hatua ya fainali ya kombe hili mwaka jana wakikutana na timu ya taifa ya Chile na kupoteza katika hatua ya matuta.
Sasa wanasubiria mshindi wa nusu fainali iliyobaki kati ya mabingwa watetezi Chile na Colombia mechi itakayochezwa Alhamisi ya tarehe 23 hapo kesho.
Goli hilo la Messi linamfanya kuwa mfungaji bora zaidi kwa Argentina akiipita rekodi ya magoli 54 iliyokuwa ikishikiliwa na Gabriel Batistuta.

Comments
Post a Comment