SAFARI YA MKHTARYAN MAN UTD YAIVA

Tetesi za kiungo mshambuliaji huyo wa Borrusia Dortmund kusajiliwa na Manchester United mashetani wekundu zashika kasi baada ya wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola kusema kuwa Manchester United ni ndoto ya Mkhitaryan.




Mkhitaryan amekuwa silaha kubwa kwa Dortmund msimu uliopita akitupia wavuni magoli 23 katika mashindano yote, assist 15 na alipigiwa kura kama mchezaji wa msimu wa msimu wa Bundesliga 2015-2016.


Super agent Mino Raiola ambaye ni wakala wa mchezaji huyu amewasaidia wachezaji wake wengine ambao ni wakala wao kuchukuliwa na timu kubwa wakiwamo Zlatan Ibrahimovic 'Ibracadabra' ,Romelu Lukaku, Paul Pogba na 'Super Mario' Mario Ballotelli.



Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia