ITALIA 'AZZURI' WALIPIKIZA KISASI KWA SPAIN

Italia wameendeleza ubabe wao kwenye mashindano ya EURO yanayoendelea Ufaransa ikiwa ni hatua ya 16 bora wakiibuka na ushindi wa goli 1-0.


Ilikuwa ni marudio ya fainali ya EURO ya mwaka 2012, Italia wakilipiza kisasi wakifungwa bao 4-0 na Spain.

 Alikuwa ni Giorgio Chiellini mnamo dakika ya 33 akiwaadhibu Spain huku Graziano Pelle akitoa matumaini yoyote ya Spain kurudisha akiwaandikia Italia bao la pili dakika ya 90.


Kwa matokeo hayo Italia watakutana na Ujerumani katika hatua ya robo fainali waliowatoa Slovakia kwa jumla ya goli 3-0.

Comments

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia