Posts

Showing posts from 2016

Magazeti ya leo, Jumapili Julai 24

Image

Haya Hapa magazeti ya leo Julai 2 2016

Image

KLOPP AMNASA MANE

Image
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Southampton Sadio Mane hatimaye baada ya tetesi za muda mrefu amesaini kandarasi ya miaka 5 na majogoo wa Anfield Liverpool kwa ada ya paundi ml 34. Mane anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Liverpool msimu huu, Klopp ameshafanya usajili wa Joel Matip na kipa Loris Karius. Klopp ameonyesha nia ya dhati ya kuwa na safu ya ushambuliaji iliyoshiba tayari yenye majina kama Benteke, Sturridge na Origi. Kwa usajili huu mashabiki wa Liverpool wanazidi kuwa na imani ya klabu yao kufanya vizuri msimu ujao ikikumbukwa Klopp aliifikisha fainali za Europa na Capital one cup bila usajili wowote.

UINGEREZA AIBU, HODGSON ATIMUA

Image
Timu ya taifa ya Uingereza ' The three Lions' imeaga fainali za EURO zinazoendelea Ufaransa baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Iceland. Uingereza ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa mshambuliaji wa Mashetani wekundu Wayne Rooney 'Wazza' dakika ya 4 kwa njia ya mkwaju wa penalti, lakini Iceland wakarudi mchezoni na kusawazisha dakika ya 6 kupitia kwa Sigurdsson na kumalizia la pili dakika ya 16 kupitia kwake Sigthorsson. Matokeo haya ya kushangaza yanamaanisha Iceland watakipiga na  Ujerumani hatua ya robo fainali baada ya kuwatoa Slovakia. Ikumbukwe mapema mwa mashindano haya Chief wa shirikisho la mpira nchini Uingereza FA bwana Greg Dyke alisema kwamba kocha mkuu Roy Hodgson atatimuliwa endapo atashindwa kuifikisha Uingereza nusu fainali. Basi kufuatia kutolewa kwa Uingereza Hodgson bila ya kutimuliwa ameamua kujivua kama kocha mkuu wa Uingereza.

ITALIA 'AZZURI' WALIPIKIZA KISASI KWA SPAIN

Image
Italia wameendeleza ubabe wao kwenye mashindano ya EURO yanayoendelea Ufaransa ikiwa ni hatua ya 16 bora wakiibuka na ushindi wa goli 1-0. Ilikuwa ni marudio ya fainali ya EURO ya mwaka 2012, Italia wakilipiza kisasi wakifungwa bao 4-0 na Spain.  Alikuwa ni Giorgio Chiellini mnamo dakika ya 33 akiwaadhibu Spain huku Graziano Pelle akitoa matumaini yoyote ya Spain kurudisha akiwaandikia Italia bao la pili dakika ya 90. Kwa matokeo hayo Italia watakutana na Ujerumani katika hatua ya robo fainali waliowatoa Slovakia kwa jumla ya goli 3-0.

BELGIUM YAWAPA KOZI YA BURE HUNGARY

Image
Ikiwa ni mwendelezo wa mechi za hatua ya 16 bora Belgium yawafungisha vilago hungary baada ya kupata ushindi mnono wa goli 4-0. Goli la kwanza liliwekwa wavuni na Toby Alberweireld mnamo dakika ya 10 na kuongeza la pili dakika ya 78 kupitia kwake Michy Batshuayi naye Hazard akiwakata maini kwa kufunga la tatu dakika ya 80, hatimaye  Carasco akipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Hungary dakika za lala salama. Kwa matokeo hayo Belgium watakutana na Wales wanaoongozwa na Gareth Bale na Ramsey Ijumaa hii, mtanange utakaopigwa kwenye dimba la Lille. Mechi nyingine zilizopigwa usiku wa leo ni Ujerumani na Slovakia, Ujerumani wakishinda 3-0, huku Antoine Griezmann akiivusha Ufaransa walioshinda 2-1 dhidi ya Ireland. Ujerumani watakutana na Italy au Spain robo fainali huku Ufaransa kumenyana na England au Iceland Jumapili ijayo.

Hii hapa Orodha kamili ya wakuu wa wilaya walioteuliwa leo

Image
Leo tarehe 26 juni 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameteua wakuu wa wilaya wapya kwa mikoa yote ya Tanzania bara. Taarifa ya uteuzi huo imetolewa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Bwn Gerson Msigwa. Na hapa chini ndio majina ya wakuu wa wilaya wote walioteuliwa leo. ARUSHA Arusha           -           Mrisho Mashaka Gambo Arumeru        -           Alexander Pastory Mnyeti Ngorongoro  -           Rashid Mfaume Taka Longido         -           Daniel Geofrey Chongolo Monduli         -         ...

RAIS MAGUFULI AMEFANYA MABADILIKO KWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA

Image
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli, Leo tar 20 juni 2016 amefanya mabadiliko katika safi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imetolewa leo na Kaimu wa mawasiliano na habari Ikulu bwana Gerson Msigwa.

Magazeti ya Tanzania leo juni 26

Image