Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi


Na: Ridhaa Korongo



Pampasi ya kwanza ilianza kutumika mnamo mwaka 1961 nchini Marekani, baada ya wazo la kutengeneza pampasi kutolewa na Mmarekani Victor Mills mwaka 1956. Hii ilitokana na kuchoshwa kwake na kazi ya kubadili nepi za mjukuu wake. Tangu wakati huo, pampasi zimeenea duniani kote, zikiwapa wazazi njia rahisi zaidi ya kudhibiti haja za watoto.

Hapa Tanzania, pampasi zilianza kutumika mapema miaka ya 2000 na zimeendelea kushamiri, hasa katika maeneo ya mijini. Kwa sasa, pampasi zimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya wazazi, zikichukua nafasi ya mipira, nepi, na matambara yaliyokuwa yakitumiwa zamani. Wakati huo, kila mzazi alihitaji kuchana vipande vya kanga au kununua nepi kwa ajili ya watoto wao. Lakini siku hizi, imekuwa kawaida kwa kila familia yenye mtoto kuwa na pampasi, ambayo sasa hutumika kama “nguo ya ndani” kwa watoto, ikisaidia kuzuia kinyesi na mkojo kutapakaa.

Ingawa pampasi zimewasaidia wazazi kwa kuwaondolea kazi kubwa ya kufua nepi na matambara mara kwa mara, je, tunaweza kusema kuwa hii ndiyo njia salama zaidi? Zamani, wazazi walilazimika kuwachunguza watoto mara kwa mara na kupanga muda wa kusafisha nepi, hali ambayo ilikuwa inakuza ukaribu na uangalizi wa karibu wa watoto.

Ni kweli pampasi zimerahisisha maisha, lakini hatupaswi kupuuza athari zake. Je, wazazi wamezingatia madhara yanayoweza kutokana na matumizi ya pampasi? Na muhimu zaidi, je, wanajua matumizi sahihi ya pampasi ili kuhakikisha usalama wa watoto wao?

Lenye faida halikosi changamoto – ni wakati wa kuangalia kwa undani zaidi namna tunavyotumia bidhaa hizi muhimu.

Matambara yalitumika kabla ya pampasi



Kwa utafiti mdogo nilioufanya, nimegundua kuwa wazazi wengi hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya pampasi kwa watoto. Wengi wao wamekuwa wakiwavisha watoto pampasi na kuendelea na shughuli zao mpaka pale watakapopata muda wa kuwabadilisha.

Nilizungumza na Latifa Khalfani, binti wa miaka 25 na mama wa mtoto mmoja. Latifa hufanya hivi: humvisha mwanawe pampasi usiku na humvua anapoamka asubuhi. “Na asubuhi nikienda naye Kariakoo namvisha tena, hiyo ndiyo mpaka saa 7 au 8, maana siwezi kusimama kwenye maduka kumbadilisha pampasi,” alisema. Huyu ni mfano tu wa hali halisi, lakini tumeshuhudia wazazi wengi hata safarini, wakimvalisha mtoto pampasi kutoka Dar es Salaam hadi Njombe bila kumbadilisha.

Hali hii ina maana kuwa mtoto anaweza kujisaidia mara kadhaa bila kubadilishiwa pampasi, na hivyo kulazimika kukaa muda mrefu na mkojo au kinyesi ndani ya pampasi yake.

Miaka ya hivi karibuni, watoto wengi wameanza kuathirika zaidi kutokana na matumizi mabaya ya pampasi. Athari hizo ni pamoja na kupata maradhi kama uchovu, kuchubuka sehemu za siri, na kudumaa kwa afya zao. Sababu kuu ya hali hii ni watoto kuvalishwa pampasi kwa muda mrefu bila kubadilishwa.

Dokta Kevin wa Dar es Salaam anabainisha kuwa kuna madhara mengi yanayoweza kumpata mtoto anayevalishwa pampasi kwa muda mrefu. Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na:

  • Magonjwa ya maambukizi kwenye njia ya mkojo (U.T.I)
  • Kuchubuka ngozi (inflammation of the skin)
  • Fangasi, zinazosababisha muwasho sehemu za siri

Magonjwa haya husababishwa na unyevu unaotokana na mkojo au kinyesi kukaa muda mrefu kwenye pampasi. Yasipotibiwa mapema, madhara hayo yanaweza kuathiri afya ya mtoto kwa kiwango kikubwa.

Kwa mfano, muwasho wa ngozi humfanya mtoto kulia mara kwa mara kwa kukosa utulivu, hali inayoweza kuathiri ukuaji wake. Vilevile, hali hii inaweza kusababisha matatizo mengine kama maumivu ya mgongo, kushindwa kufanya kazi kwa figo, na hata kuharibika kwa viungo vya uzazi.

Nilizungumza pia na mwanafunzi wa darasa la pili kutoka Shule ya Msingi Upendo, mkoani Dar es Salaam, mwenye miaka 7 lakini bado anavalishwa pampasi kutokana na tatizo lake. Mtoto huyo alikiri kuwa hapendi kabisa kuvaa pampasi kwa sababu zinakuwa na joto kali na humfanya ashindwe kulala vizuri. Mama yake pia alikiri kwamba mwanawe hapendi, lakini hulazimika kumvalisha.

Madhara ya pampasi si kwa watoto tu, bali pia kwa mazingira. Pampasi, zikiwa zimetengenezwa kwa karatasi na nailoni ambazo huchukua muda mrefu kuoza, zimekuwa chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira. Wazazi wengine hutupa pampasi ovyo katika maeneo ya wazi au kwenye mashimo ya takataka, na pampasi hizo zikiingia kwenye vyanzo vya maji, husababisha magonjwa kama kipindupindu, kichocho, na kuhara damu.

Baada ya yote hayo, swali linabaki: matumizi sahihi ya pampasi ni yapi? Dokta Mtali anashauri kuwa pampasi inapaswa kubadilishwa mara tu mtoto anapojisaidia. Hata kama hajajisaidia, haifai mtoto avae pampasi moja kwa muda mrefu, achilia mbali kutwa nzima.

Hii ina maana kwamba wazazi wanapaswa kuwa makini kuangalia watoto mara kwa mara ili kubaini ikiwa wamejisaidia na kuwabadilisha haraka. Si vyema mtoto kukaa na mkojo au kinyesi kwenye pampasi kwa saa nzima.

Kwa karne ya sasa, si rahisi kuzuia matumizi ya pampasi, lakini serikali inapaswa kuhakikisha kuwa ni pampasi zenye ubora wa hali ya juu ndizo zinazoingizwa nchini. Aidha, wazazi na walezi wanapaswa kuhakikisha watoto wao hawakai na pampasi moja kwa muda mrefu.

Pia, ni muhimu kuhakikisha kuwa pampasi zilizotumika zinahifadhiwa au kutupwa katika njia sahihi ili kuepusha madhara yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.

Comments

  1. Cha msingi hapa ni suala la elimu juu ya matumizi ya pampas, hivyo wizara ya afya pamoja na wadau mbali mbali wa masuala ya "Afya ya mama na mtoto"kuwa na jukumu la kuielimisha jamii hasa akina mama juu ya madhara yatokanayo na kifaa hiki kwa kutozingatia usafi.
    Ahsanten naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  2. Sasa kila kitu kina madhara

    ReplyDelete
  3. Kusema ukweli me nilikuwa siyafahamu madhara ya pampas ila baada ya kuambiwa na watu ikabidi niingie mtandao nakuyafahamu meng zaid asanteni sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Me nimeambiwa watoto mtoto wa kiume akivalishwa pampas anakosa nguvu za kiume ndo nikaja kuhakiki ila watu wanajua kukuza mambo πŸ˜ƒπŸ˜ƒ

      Delete
    2. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£hata mim niliambiwaga ivo jmn

      Delete
  4. Yaani mpaka watu wanaogopa Sasa kweli kunakitakachotumika kweli maana jamani?hebu tupeni tu muongozo

    ReplyDelete
  5. I'ts ok!! So all parents we must be carefull for our babies. & no other wise!!!!!

    ReplyDelete
  6. Nashukuru kwa ushauri mzuri! Cha msingi ni kujitaidi kuwa makini na kumuangalia mtoto kila mara

    ReplyDelete
  7. Mwanangu wa kiume alikua anasimamisha uboo wake vizuri,hivi karibuni hasimamishi Tena. Je? Matumiz ya pampas yanaweza kua in chanzo???

    ReplyDelete
  8. Usasa unatuumiza wazazi mtoto akikua ndio tutayaona madhara yake

    ReplyDelete
  9. Serikali na wizara ya afya waone umuhimu wa kuwa na viwanda vingi vya pampasi ziuzwe kwa bei nafuu sana watoto wavae kwa wingi yaani nyingi kwa siku hata 15

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia