Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi
Pampasi ya kwanza ilianza kutumika mnamo mwaka 1961 nchini Marekani, baada ya wazo la kutengeneza pampasi kutolewa na Mmarekani Victor Mills mwaka 1956. Hii ilitokana na kuchoshwa kwake na kazi ya kubadili nepi za mjukuu wake. Tangu wakati huo, pampasi zimeenea duniani kote, zikiwapa wazazi njia rahisi zaidi ya kudhibiti haja za watoto.
Hapa Tanzania, pampasi zilianza kutumika mapema miaka ya 2000 na zimeendelea kushamiri, hasa katika maeneo ya mijini. Kwa sasa, pampasi zimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya wazazi, zikichukua nafasi ya mipira, nepi, na matambara yaliyokuwa yakitumiwa zamani. Wakati huo, kila mzazi alihitaji kuchana vipande vya kanga au kununua nepi kwa ajili ya watoto wao. Lakini siku hizi, imekuwa kawaida kwa kila familia yenye mtoto kuwa na pampasi, ambayo sasa hutumika kama “nguo ya ndani” kwa watoto, ikisaidia kuzuia kinyesi na mkojo kutapakaa.
Ingawa pampasi zimewasaidia wazazi kwa kuwaondolea kazi kubwa ya kufua nepi na matambara mara kwa mara, je, tunaweza kusema kuwa hii ndiyo njia salama zaidi? Zamani, wazazi walilazimika kuwachunguza watoto mara kwa mara na kupanga muda wa kusafisha nepi, hali ambayo ilikuwa inakuza ukaribu na uangalizi wa karibu wa watoto.
Ni kweli pampasi zimerahisisha maisha, lakini hatupaswi kupuuza athari zake. Je, wazazi wamezingatia madhara yanayoweza kutokana na matumizi ya pampasi? Na muhimu zaidi, je, wanajua matumizi sahihi ya pampasi ili kuhakikisha usalama wa watoto wao?
Lenye faida halikosi changamoto – ni wakati wa kuangalia kwa undani zaidi namna tunavyotumia bidhaa hizi muhimu.
![]() |
Matambara yalitumika kabla ya pampasi |
Kwa utafiti mdogo nilioufanya, nimegundua kuwa wazazi wengi hawana elimu ya
kutosha juu ya matumizi sahihi ya pampasi kwa watoto. Wengi wao wamekuwa
wakiwavisha watoto pampasi na kuendelea na shughuli zao mpaka pale watakapopata
muda wa kuwabadilisha.
Nilizungumza na Latifa Khalfani, binti wa miaka 25 na mama wa mtoto mmoja.
Latifa hufanya hivi: humvisha mwanawe pampasi usiku na humvua anapoamka
asubuhi. “Na asubuhi nikienda naye Kariakoo namvisha tena, hiyo ndiyo mpaka saa
7 au 8, maana siwezi kusimama kwenye maduka kumbadilisha pampasi,” alisema.
Huyu ni mfano tu wa hali halisi, lakini tumeshuhudia wazazi wengi hata
safarini, wakimvalisha mtoto pampasi kutoka Dar es Salaam hadi Njombe bila
kumbadilisha.
Hali hii ina maana kuwa mtoto anaweza kujisaidia mara kadhaa bila
kubadilishiwa pampasi, na hivyo kulazimika kukaa muda mrefu na mkojo au kinyesi
ndani ya pampasi yake.
Miaka ya hivi karibuni, watoto wengi wameanza kuathirika zaidi kutokana na
matumizi mabaya ya pampasi. Athari hizo ni pamoja na kupata maradhi kama
uchovu, kuchubuka sehemu za siri, na kudumaa kwa afya zao. Sababu kuu ya hali
hii ni watoto kuvalishwa pampasi kwa muda mrefu bila kubadilishwa.
Dokta Kevin wa Dar es Salaam anabainisha kuwa kuna madhara mengi yanayoweza
kumpata mtoto anayevalishwa pampasi kwa muda mrefu. Baadhi ya madhara hayo ni
pamoja na:
- Magonjwa ya maambukizi kwenye njia ya mkojo (U.T.I)
- Kuchubuka ngozi (inflammation of the skin)
- Fangasi, zinazosababisha muwasho sehemu za siri
Magonjwa haya husababishwa na unyevu unaotokana na mkojo au kinyesi kukaa
muda mrefu kwenye pampasi. Yasipotibiwa mapema, madhara hayo yanaweza kuathiri
afya ya mtoto kwa kiwango kikubwa.
Kwa mfano, muwasho wa ngozi humfanya mtoto kulia mara kwa mara kwa kukosa
utulivu, hali inayoweza kuathiri ukuaji wake. Vilevile, hali hii inaweza
kusababisha matatizo mengine kama maumivu ya mgongo, kushindwa kufanya kazi kwa
figo, na hata kuharibika kwa viungo vya uzazi.
Nilizungumza pia na mwanafunzi wa darasa la pili kutoka Shule ya Msingi
Upendo, mkoani Dar es Salaam, mwenye miaka 7 lakini bado anavalishwa pampasi
kutokana na tatizo lake. Mtoto huyo alikiri kuwa hapendi kabisa kuvaa pampasi
kwa sababu zinakuwa na joto kali na humfanya ashindwe kulala vizuri. Mama yake
pia alikiri kwamba mwanawe hapendi, lakini hulazimika kumvalisha.
Madhara ya pampasi si kwa watoto tu, bali pia kwa mazingira. Pampasi,
zikiwa zimetengenezwa kwa karatasi na nailoni ambazo huchukua muda mrefu kuoza,
zimekuwa chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira. Wazazi wengine hutupa
pampasi ovyo katika maeneo ya wazi au kwenye mashimo ya takataka, na pampasi
hizo zikiingia kwenye vyanzo vya maji, husababisha magonjwa kama kipindupindu,
kichocho, na kuhara damu.
Baada ya yote hayo, swali linabaki: matumizi sahihi ya pampasi ni yapi?
Dokta Mtali anashauri kuwa pampasi inapaswa kubadilishwa mara tu mtoto
anapojisaidia. Hata kama hajajisaidia, haifai mtoto avae pampasi moja kwa muda
mrefu, achilia mbali kutwa nzima.
Hii ina maana kwamba wazazi wanapaswa kuwa makini kuangalia watoto mara kwa
mara ili kubaini ikiwa wamejisaidia na kuwabadilisha haraka. Si vyema mtoto
kukaa na mkojo au kinyesi kwenye pampasi kwa saa nzima.
Kwa karne ya sasa, si rahisi kuzuia matumizi ya pampasi, lakini serikali
inapaswa kuhakikisha kuwa ni pampasi zenye ubora wa hali ya juu ndizo
zinazoingizwa nchini. Aidha, wazazi na walezi wanapaswa kuhakikisha watoto wao
hawakai na pampasi moja kwa muda mrefu.
Pia, ni muhimu kuhakikisha kuwa pampasi zilizotumika zinahifadhiwa au
kutupwa katika njia sahihi ili kuepusha madhara yatokanayo na uchafuzi wa
mazingira.
Cha msingi hapa ni suala la elimu juu ya matumizi ya pampas, hivyo wizara ya afya pamoja na wadau mbali mbali wa masuala ya "Afya ya mama na mtoto"kuwa na jukumu la kuielimisha jamii hasa akina mama juu ya madhara yatokanayo na kifaa hiki kwa kutozingatia usafi.
ReplyDeleteAhsanten naomba kuwasilisha.
Sasa kila kitu kina madhara
ReplyDeleteUmakini tu na uvivu uepukwe
ReplyDeleteKusema ukweli me nilikuwa siyafahamu madhara ya pampas ila baada ya kuambiwa na watu ikabidi niingie mtandao nakuyafahamu meng zaid asanteni sana
ReplyDeleteMe nimeambiwa watoto mtoto wa kiume akivalishwa pampas anakosa nguvu za kiume ndo nikaja kuhakiki ila watu wanajua kukuza mambo ππ
Deleteπππ€£hata mim niliambiwaga ivo jmn
DeleteYaani mpaka watu wanaogopa Sasa kweli kunakitakachotumika kweli maana jamani?hebu tupeni tu muongozo
ReplyDeleteI'ts ok!! So all parents we must be carefull for our babies. & no other wise!!!!!
ReplyDeleteNashukuru kwa ushauri mzuri! Cha msingi ni kujitaidi kuwa makini na kumuangalia mtoto kila mara
ReplyDeleteMwanangu wa kiume alikua anasimamisha uboo wake vizuri,hivi karibuni hasimamishi Tena. Je? Matumiz ya pampas yanaweza kua in chanzo???
ReplyDeleteNdio ni Sababu pia
Deleteπ€
ReplyDeleteUsasa unatuumiza wazazi mtoto akikua ndio tutayaona madhara yake
ReplyDeleteSerikali na wizara ya afya waone umuhimu wa kuwa na viwanda vingi vya pampasi ziuzwe kwa bei nafuu sana watoto wavae kwa wingi yaani nyingi kwa siku hata 15
ReplyDelete