Posts

Showing posts from June, 2016

KLOPP AMNASA MANE

Image
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Southampton Sadio Mane hatimaye baada ya tetesi za muda mrefu amesaini kandarasi ya miaka 5 na majogoo wa Anfield Liverpool kwa ada ya paundi ml 34. Mane anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Liverpool msimu huu, Klopp ameshafanya usajili wa Joel Matip na kipa Loris Karius. Klopp ameonyesha nia ya dhati ya kuwa na safu ya ushambuliaji iliyoshiba tayari yenye majina kama Benteke, Sturridge na Origi. Kwa usajili huu mashabiki wa Liverpool wanazidi kuwa na imani ya klabu yao kufanya vizuri msimu ujao ikikumbukwa Klopp aliifikisha fainali za Europa na Capital one cup bila usajili wowote.

UINGEREZA AIBU, HODGSON ATIMUA

Image
Timu ya taifa ya Uingereza ' The three Lions' imeaga fainali za EURO zinazoendelea Ufaransa baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Iceland. Uingereza ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa mshambuliaji wa Mashetani wekundu Wayne Rooney 'Wazza' dakika ya 4 kwa njia ya mkwaju wa penalti, lakini Iceland wakarudi mchezoni na kusawazisha dakika ya 6 kupitia kwa Sigurdsson na kumalizia la pili dakika ya 16 kupitia kwake Sigthorsson. Matokeo haya ya kushangaza yanamaanisha Iceland watakipiga na  Ujerumani hatua ya robo fainali baada ya kuwatoa Slovakia. Ikumbukwe mapema mwa mashindano haya Chief wa shirikisho la mpira nchini Uingereza FA bwana Greg Dyke alisema kwamba kocha mkuu Roy Hodgson atatimuliwa endapo atashindwa kuifikisha Uingereza nusu fainali. Basi kufuatia kutolewa kwa Uingereza Hodgson bila ya kutimuliwa ameamua kujivua kama kocha mkuu wa Uingereza.

ITALIA 'AZZURI' WALIPIKIZA KISASI KWA SPAIN

Image
Italia wameendeleza ubabe wao kwenye mashindano ya EURO yanayoendelea Ufaransa ikiwa ni hatua ya 16 bora wakiibuka na ushindi wa goli 1-0. Ilikuwa ni marudio ya fainali ya EURO ya mwaka 2012, Italia wakilipiza kisasi wakifungwa bao 4-0 na Spain.  Alikuwa ni Giorgio Chiellini mnamo dakika ya 33 akiwaadhibu Spain huku Graziano Pelle akitoa matumaini yoyote ya Spain kurudisha akiwaandikia Italia bao la pili dakika ya 90. Kwa matokeo hayo Italia watakutana na Ujerumani katika hatua ya robo fainali waliowatoa Slovakia kwa jumla ya goli 3-0.

BELGIUM YAWAPA KOZI YA BURE HUNGARY

Image
Ikiwa ni mwendelezo wa mechi za hatua ya 16 bora Belgium yawafungisha vilago hungary baada ya kupata ushindi mnono wa goli 4-0. Goli la kwanza liliwekwa wavuni na Toby Alberweireld mnamo dakika ya 10 na kuongeza la pili dakika ya 78 kupitia kwake Michy Batshuayi naye Hazard akiwakata maini kwa kufunga la tatu dakika ya 80, hatimaye  Carasco akipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Hungary dakika za lala salama. Kwa matokeo hayo Belgium watakutana na Wales wanaoongozwa na Gareth Bale na Ramsey Ijumaa hii, mtanange utakaopigwa kwenye dimba la Lille. Mechi nyingine zilizopigwa usiku wa leo ni Ujerumani na Slovakia, Ujerumani wakishinda 3-0, huku Antoine Griezmann akiivusha Ufaransa walioshinda 2-1 dhidi ya Ireland. Ujerumani watakutana na Italy au Spain robo fainali huku Ufaransa kumenyana na England au Iceland Jumapili ijayo.

Hii hapa Orodha kamili ya wakuu wa wilaya walioteuliwa leo

Image
Leo tarehe 26 juni 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameteua wakuu wa wilaya wapya kwa mikoa yote ya Tanzania bara. Taarifa ya uteuzi huo imetolewa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Bwn Gerson Msigwa. Na hapa chini ndio majina ya wakuu wa wilaya wote walioteuliwa leo. ARUSHA Arusha           -           Mrisho Mashaka Gambo Arumeru        -           Alexander Pastory Mnyeti Ngorongoro  -           Rashid Mfaume Taka Longido         -           Daniel Geofrey Chongolo Monduli         -         ...

RAIS MAGUFULI AMEFANYA MABADILIKO KWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA

Image
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli, Leo tar 20 juni 2016 amefanya mabadiliko katika safi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imetolewa leo na Kaimu wa mawasiliano na habari Ikulu bwana Gerson Msigwa.

Magazeti ya Tanzania leo juni 26

Image

Diamond Platnumz akosa tuzo aliyoshiriki BET

Image
Macho na Maskio ya Watanzania wengi yalikua yameekea kwenye tuzo za BET 2016 zilizokua zikitolewa Usiku wa Tar 26 juni huko Los Angels nchini Marekani. Japo kulikua na vipenge vingi lakin kilichokua kikisubiriwa kwa hamu ni kile cha Best International Act ambacho Mtanzania Diamond Platnumz alikuwa akishindana na wasanii wengine kama AKA (South Africa), Wizkid (Nigeria), Serge Beynaud (Ivory Coast) MzVee (Ghana), Cassper Nyovest (South Africa),Black Coffee (South Africa) na Yemi Alade (Nigeria). lakini kwa bahati mbaya Diamond Platnumz hakufanikiwa kupata tuzo hiyo na badala yake msanii Black Coffee kutoka South Africa ndiye aliyeshinda tuzo hiyo na kutangazwa kuwa msindi wa BET Awards Best International Act: Africa 2016.                                                                Black Coffee Mashabiki we...

CR7 KWA MBINDE ROBO FAINALI EURO

Image
Imechukua dakika 30 za nyongeza ndipo Portugal walipoweza kuchomoza na ushindi finyu wa bao moja, bao lililofungwa na Ricardo Quaresma mnamo dakika ya 117 ya mchezo. Matokeo hayo yanaipeleka Ureno robo fainali wakikutana na Poland walioitoa Switzerland kwenye mechi nyingine iliyopigwa mapema usiku wa leo. Ni robo fainali inayosubiriwa kwa hamu ikikutanisha washambuliaji wawili wenye majina na mafanikio katika klabu zao, Cristiano ronaldo 'CR7' anyekipiga Real Madrid kwa Ureno na Robert Lewandowski anayekipiga kunako Bayern Munchen 'The Bavarians'.

BALE RAMSEY WATINGA ROBO FAINALI EURO

Image
Robo fainali ya pili imepigwa usiku wa leo kati ya Wales na Northern Ireland katika dimba la Parc Des Princes, Wales wakipata ushindi mwembamba wa goli 1-0. Bao hilo pekee la mchezo lilifungwa mnamo dakika ya 75 ya mchezo na Gareth McAuley likiwa ni la kujifunga, goli lililodumu mpaka kipenga cha mwisho cha mchezo. Kwa matokeo hayo Wales wametinga robo fainali na wanamsubiria mshindi kati ya Hungary na Belgium, mtanange utakaopigwa Ijumaa hii katika dimba la Lille.

SERIKALI YASITISHA HUDUMA ZA VYAKULA MUHIMBILI

Image
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesitisha zoezi la utoaji chakula kwa wagonjwa hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka hapo serikali itakapojiridhisha faida na hasara ya zoezi hilo. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa amefikia maamuzi hayo baada ya kupokea maoni kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Muhimbili imeanzisha utaratibu utakaowezesha wagonjwa kuchangia gharama ya chakula ili chakula kiweze kuandaliwa na hospitali badala ya utaratibu wa sasa. Waziri huyo ameagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpaka hapo zitakapopatikana taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu huo mpya uliopendekezwa.

XHAKA SWITZERLAND WAAGA EURO

Image
Ikiwa ni mechi ya ufunguzi ya hatua ya 16 bora ya michuano ya EURO inayoendelea nchini ufaransa kati ya Switzerland na Poland, mtanange umeisha kwa Poland kupita kwa ushindi wa matuta wa penalti 5-4 . Poland walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 39 ya mchezo kupitia kwa Jakub Blaszczykowski na kujihakikishia ushindi mpaka pale Switzerland walipochomoa dakika za lala salama kupitia kwa tegemezi lao Xherdan Shaqiri dakika ya 82. Sare hiyo ililazimisha kuongezwa kwa dakika 30 lakini mpaka kufikia dakika 120 matokeo yalibaki yaleyale ya 1-1. Ulikuwa ni mkwaju wa penalti aliokosa kiungo mpya wa Arsenal Granit Xhaka ulioupa ushindi Poland na kuivusha kuingia hatua ya robo fainali. Poland watakutana na Portugal au Croatia hatua ya robo fainali, mechi kati ya Portugal na Croatia inachezwa usiku wa leo.

MZEE WENGER AHAHA

Image
Baada ya kumkosa Jamie Vardy aliyeongeza mkataba na Leicester City sasa kocha mkuu wa Arsenal the gunners washika bunduki Aresene Wenger, anahamishia nguvu kwa kiungo wa Leicester N'golo Kante. Vardy alikataa kutua Emirates waliokuwa wakitaka kumnunua kwa kitita cha paundi millioni ishirini na kubaki King power stadium baada ya kuongezewa mshahara kufikia paundi laki moja kwa wiki. Kwa miaka ya karibuni, Wenger amekuwa na historia ya kupokonywa tonge mdomoni kwa upande wa washambuliaji akikosa washambuliaji hatari kama Luis Suarez, Gonzalo Higuain, Wayne Rooney, Karim Benzema na sasa Jamie Vardy.

FURY VS KLITSCHKO YAOTA MBAWA

Image
Mpambano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kati ya Klitschko na Fury uliokuwa upiganwe mnamo tarehe 9 julai mwaka huu katika mji wa Manchester jijini London, umeghairishwa baada ya Fury kuumia kifundo cha mguu akifanya mazoezi. Hii ni mara ya pili kukutana wanamasumbwi hawa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi November mwaka jana ambapo Fury alimtwanga Klitschko na kutwaa ubingwa wa uzito wa juu wa dunia. Mwingereza Tyson fury 'THE FURIOUS ONE'  amepigana mapambano 25 akishinda yote huku 18 kati ya hayo akishinda kwa KO.

Maelfu wachaguliwa kujiunga kidato cha tano 2016

Image
Serikali kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2016. Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi . Aidha ripoti hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa TAMISEMI inasema kuwa wanafunzi hao   waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi. Kusoma majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano << BOFYA HAPA >>

Heslb imetoa muongozo wa kuomba mkopo

Image
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini imetoa kitabu cha muongozo (maelekezo) ya kuomba mkopo kwa mwaka wa masomo 2016/17. Aidha bodi hiyo imetangaza muda wa kupokea maombi ya mkopo ambayo ni kuanzia tar 27 juni mpaka tar 31 julai mwaka huu na pia lazima maombi yote yafanyike kwa njia ya mtandao kwa kupitia mfumo maalum wa maombi kwa njia ya mtandao. Pia kwenye kitabu hiko zimetajwa kozi zenye vipaumbele na zile ambazo hazijapewa vipaumbele kwa mwaka huu. Bonyeza hapa kwa maelezo zaid i Bonyeza hapa ili kusoma na kudownlod kitabu cha HESLB

WIZARA YA AFYA YASITISHA HUDUMA YA CHAKULA MUHIMBILI

Image
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesitisha zoezi la utoaji chakula kwa wagonjwa hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka hapo serikali itakapojiridhisha faida na hasara ya zoezi hilo. . ------------------------------ Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema, -  Hata hivyo nimepokea maoni mengi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo itaanzisha utaratibu utakaowezesha wagonjwa kuchangia gharama ya chakula ili chakula kiweze kuandaliwa na hospitali badala ya utaratibu wa sasa’ - Kufuatia hali hii kuleta wasiwasi kwa wananchi na wagonjwa, nimeagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpak hapo tutakapopata taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu mpya unaopendekezwa’ Hii inakuja baada ya malalamiko ya baadhi ya  watu kuhusu ubora wa Huduma za vyakula hospitalini apo.  Akiongea na jopo la waandishi wa habari Leo jijini Dar es saalam ,Waziri huyo akiweka bayana Msimamo wa Ser...

EURO yafikia 16 bora

Image
Michuano ya mataifa ya Ulaya au EURO jana imemalizika kwa hatua ya makundi na timu 16 zimefuzu kwa hatua ya mtoano. hatua hiyo ya mtoano itaanza Jumamosi ya tar 25 juni kwa mechi kadhaa kupigwa siku hiyo.                                      Jinsi ambavyo hatua ya 16 bora mpaka fainali itakavochezwa

Raia wa Uingereza kupiga kura ya maoni

Image
Leo raia wa Uingereza watapiga kura ya maoni ili kufanya maamuzi ya kubaki au kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya (EU). Uingereza ilifikia uamuzi huo baada ya kuwa na mgogoro wa muda mrefu kutoka kwa wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa wakitaka Uingereza kujiondoa kwenye umoja huo. Na pia kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Waziri mkuu David Cameroon aliahidi kupigwa kwa kura hiyo wakati wa kampeni zake. Kumekua na pande mbili ambapo upande mmoja ukitaka nchi hiyo isalie kwenye umoja huo huku upande huo wa pili ukitaka nchi hiyo kujiondoa. David Cameroon akiwa kwenye kampeni za kutaka Uingereza isalie EU.

Soma magazeti ya leo tar 23 juni 2016

Image