XHAKA SWITZERLAND WAAGA EURO

Ikiwa ni mechi ya ufunguzi ya hatua ya 16 bora ya michuano ya EURO inayoendelea nchini ufaransa kati ya Switzerland na Poland, mtanange umeisha kwa Poland kupita kwa ushindi wa matuta wa penalti 5-4 .

Poland walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 39 ya mchezo kupitia kwa Jakub Blaszczykowski na kujihakikishia ushindi mpaka pale Switzerland walipochomoa dakika za lala salama kupitia kwa tegemezi lao Xherdan Shaqiri dakika ya 82.

Sare hiyo ililazimisha kuongezwa kwa dakika 30 lakini mpaka kufikia dakika 120 matokeo yalibaki yaleyale ya 1-1.

Ulikuwa ni mkwaju wa penalti aliokosa kiungo mpya wa Arsenal Granit Xhaka ulioupa ushindi Poland na kuivusha kuingia hatua ya robo fainali.


Poland watakutana na Portugal au Croatia hatua ya robo fainali, mechi kati ya Portugal na Croatia inachezwa usiku wa leo.






Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Tuwalinde watoto wetu na madhara yatokanayo na Pempasi

Mwanamke na Uongozi

Unyanyasaji wa Kijinsia